NGM257

YKEEBENDA kushiriki kwenye uzinduzi wa Album ya Masterland

Spread the love

Mkali wa Munakampala, YKEEBENDA tayari ashathibitishwa kuwa atakuwa kwenye Uzindi wa Album ya Materland tarehe 23 juni 2019 kwenye viwanja vya LACOSTA BEACH.

Ikiwa watu wengi wamesubiria kwa hamu kubwa uzinduzi wa ALBUM ya kwanza yak wake mkali wa miondoka ya Afro-pop na Zouk, MASTERLAND tayari amemuongeza YKEEBENDA kutoka Uganda kwenye idadi ya wasanii ambao wataburudisha wananchi wa Burundi kwenye uzinduzi wa album hiyo iliyopachikwa jina la EGO.

Watu wengi walikuwa wakisubiri kwa hamu msanii kutoka Afrika Mashariki ambae atakuja kuambatana na wasanii wengine wa Burundi kwenye uzinduzi huo, ikiwa bado MASTERLAND alikuwa bado hajaweka wazi msanii amabae atakuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo.

Wasanii ambao watashiriki kwenye uzinduzi huo

Uzinduzi huo utawakutanisha wasanii wakali kutoka Burundi kama SAT B, VICHOU, DR CLAUDE, DOUBLE JAY, ARNOVIC, MOMO MELODY, JADIX na MASTERLAND mwenyewe.

Uzinduzi huo utafanyikiwa kwenye viwanja vya LACOSTA BEACH tarehe, 23 Juni, 2019.

Kiingilio wamekuwekea 3000FBU kwa kawaida, na 1000FBU kwa VIP.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP2Social Auto Publish Powered By : XYZScripts.com